Makubaliano ya Kisheria
Vigezo na Masharti ya Huduma
SokoSupa Technologies Limited • Masharti ya Matumizi ya Jukwaa
Masharti na Vigezo vya Matumizi ya SokoSupa
Tarehe ya Kuanza Kutumika: 06 Oktoba 2026
Karibu SokoSupa ("sisi", "yetu", au "SokoSupa"). Kwa kutumia tovuti yetu (sokosupa.com) au programu yetu ya simu (App), unakubaliana na Masharti na Vigezo hivi vya Huduma. Ikiwa hukubaliani na masharti haya, tafadhali usitumie mfumo huu.
1. MATUMIZI YA MFUMO NA AKAUNTI
- Kigezo cha Umri: Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili kufungua akaunti na kufanya biashara.
- Usalama wa Nywila: Una jukumu la kulinda nenosiri (password) lako. Shughuli zote zinazofanyika kupitia akaunti yako ni wajibu wako kisheria.
- Akaunti Moja Tu: Mtumiaji anaruhusiwa kuwa na akaunti moja tu. Ni marufuku kufungua akaunti nyingi kwa lengo la kurudia matangazo au kukwepa vizuizi vya mfumo.
2. KANUNI ZA MATANGAZO NA BEI
- Uhalisia wa Bei: Bei ya bidhaa lazima iwe halisi na sahihi. Ni marufuku kuweka bei za uongo (kama TZS 1 au bure) kwa nia ya kupotosha wanunuzi.
- Namba Inayopatikana: Namba ya simu iliyowekwa kwenye tangazo lazima iwe inapatikana hewani na ipokee simu na jumbe. Matangazo yenye namba zilizofungwa yanaweza kuondolewa mara moja.
- Bidhaa Zilizopigwa Marufuku: Ni marufuku kutangaza:
- Bidhaa ghushi au feki (counterfeits).
- Silaha, vilipuzi, au vifaa vya kijeshi.
- Dawa za kulevya au madawa yasiyo na vibali vya mamlaka za serikali.
- Picha zisizo na maadili, za ngono, au picha zilizoibwa mtandaoni.
- Haki ya Kufuta Tangazo: SokoSupa inahifadhi haki ya kufuta, kurekebisha, au kuzuia tangazo lolote wakati wowote bila kulazimika kutoa ufafanuzi au sababu kwa muuzaji.
3. MALIPO YA HUDUMA (BOOSTED ADS NA VIFURUSHI)
- Sera ya Kutorudishiwa Pesa (No-Refund): Malipo yote ya kupandisha matangazo hadhi ("Boosted Ads") au vifurushi vya wauzaji ni ya mwisho na hayarudishwi (non-refundable) chini ya mazingira yoyote.
- Ukiukaji wa Sheria: Iwapo tangazo lako la kulipia litafutwa au akaunti yako kufungiwa kwa sababu ya kuweka bidhaa haramu au udanganyifu, hutakuwa na haki ya kurejeshewa pesa yoyote.
4. USALAMA WA MIAMALA NA KANUNI YA DHAHABU (SAFETY FIRST)
- SokoSupa Si Mhusika wa Mauzo: SokoSupa inatoa tu jukwaa la kidijitali la kuwakutanisha watu. Sisi si wauzaji, si wasafirishaji, na hatushiriki kwenye mkataba wa mauzo kati ya mnunuzi na muuzaji.
- UKAGUZI WA BIDHAA NA MALIPO:
- Kamwe usitume pesa mapema (Advance Payment / Nauli / Amana) kabla ya kuonana na muuzaji uso kwa uso na kuikagua bidhaa.
- Kutana na muuzaji au mnunuzi sehemu za wazi za umma zenye usalama wakati wa mchana.
- Migogoro Kati ya Watumiaji: SokoSupa haina wajibu wa kisheria kuingilia, kusuluhisha, au kulipa fidia kwa mgogoro wowote wa kibiashara unaotokea kati ya mnunuzi na muuzaji.
5. ADHABU ZA UTAPELI NA USHIRIKIANO NA POLISI
- Kufungiwa Moja kwa Moja (Permanent Ban): Ukibainika kufanya utapeli, kuweka picha za uongo, au kuuza bidhaa za wizi, akaunti yako itafungwa moja kwa moja bila onyo.
- Kukabidhi Data kwa Jeshi la Polisi: Chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Tanzania (Cybercrimes Act, 2015), SokoSupa itatoa namba ya simu, anwani ya IP, na kumbukumbu zote za mtuhumiwa kwa Jeshi la Polisi na mamlaka za sheria bila taarifa kwa mtuhumiwa.
6. KUKANUSHA DHAMANA NA UKOMO WA DHIMA (LIMITATION OF LIABILITY)
- Hali ya Bidhaa ("As-Is"): Huduma za SokoSupa na bidhaa zote zinazotangazwa zinatolewa "kama zilivyo" (As-Is) bila dhamana yoyote ya ubora, usalama, au uhalali wake.
- Ukomo wa Dhima: SokoSupa haitahusika na hasara yoyote ya kifedha, madhara, au upotevu unaotokana na makubaliano binafsi kati ya watumiaji. Dhima ya juu kabisa ya SokoSupa kwa madai yoyote ya kibiashara haitazidi kiasi ambacho mtumiaji alilipa kwa huduma ya tangazo (Boost) katika miezi 3 iliyopita.
7. LESENI YA MAUDHUI NA MASOKO
Unapopakia picha na maelezo ya bidhaa, unabaki kuwa mmiliki wa maudhui yako, lakini unatupa SokoSupa leseni ya bure ya kutumia picha na maelezo hayo kuitangaza bidhaa yako kwenye mitandao ya kijamii (Instagram, Facebook, n.k.) na kampeni zetu za kibiashara.
8. SHERIA INAYOTUMIKA (GOVERNING LAW)
Masharti haya yanasimamiwa na kufasiriwa kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
9. Mabadiliko ya Masharti na vigezo vya matumizi
9. Mabadiliko ya Masharti na vigezo vya matumizi
Tunaweza kuboresha masharti na vigezo vya matumizi ya jukwaa la Sokosupa mara kwa mara. Mabadiliko makubwa yatakapotokea, tutakujulisha kupitia programu ya simu, barua pepe, au tovuti kabla hayajaanza kutumika rasmi.
10. WASILIANA NASI
- Jina la Kampuni: SokoSupa Company Limited
- Barua Pepe: support@sokosupa.com
- Simu ya Huduma: +255 771 149 149
- Anuani ya Ofisi: Kariakoo, Dar es Salaam, Tanzania
Una Swali Kuhusu Masharti Haya?
Wasiliana na timu yetu ya kisheria na usaidizi wa wateja: